Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi wilayani Hai
(UVCCM), Arnold Swai amepinga ya kurejea ndani ya chama hicho kwa
mwanadiplomasia na mwanasiasa mkongwe nchini, Balozi Juma Mwapachu.
Balozi Mwapachu, juzi alitangaza kurejea CCM kwa madai ya kuridhishwa na utendaji wa Rais Magufuli.
Akizungumza na wanahabari jana mkoani hapa,Swai alisema kuwa chama
hakipaswi kumpokea mwanasiasa huyo kwa madai kuwa ni msaliti huku
akienda mbele zaidi na kutaka waliompokea wachukuliwe hatua za kinidhamu
kwa mujibu wa kanuni za chama.
“Ni lazima tujiulize, hivi mwanadiplomasia huyo angekuwa tayari
kurejea CCM kama mgombea urais wa UKAWA, Edward Lowassa angeshinda
urais?” alihoji na kuongeza:
“Hatuwezi kumpokea msaliti kama huyu, wakati chama kilipokuwa kwenye
mapambano aliondoka tena kwa kejeli, leo chama chetu kimesimama imara
chini ya mwenyekiti wetu Rais mstaafu Jakaya Kikwete, ndio anarudi na
wimbo uleule kwamba chama kimemlea, haikubaliki.”
Alisema wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,baadhi
ya makada maarufu wa CCM walikisaliti chama huku wakitoa kauli za
kejeli na kusababisha mpasuko ndani ya chama ambao majeraha yake
hayajapona.
Mwenyekiti huyo alieleza kukerwa na kauli ya Balozi Mwapachu kwamba
chama ndo kimemlea na kwamba hayo si maradhi ya kumuua mtu bali
yanatibika, lakini dhambi ya usaliti haitibiki
“Nguvu kubwa iliyotumiwa na CCM kuwanadi wagombea wake ilisababishwa
na wasaliti kama hawa,nawaomba viongozi wa ngazi za juu kutofumbia macho
jambo hili kwani ni hatari kwa ustawi wa chama chetu.” Alisema
Balozi Mwapachu alirejea CCM juzi na kupokelwa na mwenyekiti wa CCM
kata ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, Athuman Mareenda, ambaye
alimkabidhi tena kadi ya uanachama wa chama hicho.
Chanzo: Mpekuzi
Comments