Msichana wa miaka 17 amejifungulia chooni katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam Msichana wa umri wa miaka 17 ambaye alikuwa katika machungu ya uzazi, amejikuta akijifungulia mtoto chooni baada ya muuguzi mmoja wa Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam kumtaka aende kuoga na kubadilisha nguo bila ya kujali hali yake. Msichana huyo, Asha Sudi (17), mkazi wa Tabata Kisiwani, alikutwa na tukio hilo juzi wakati akisubiri kujifungua, na uongozi wa Amana umesema utalishughulikia suala hilo. Asha alisema alifika hospitalini hapo saa 4:00 asubuhi akiwa anaumwa na uchungu na alipofika mapokezi alikalishwa kwenye benchi. “Wakati nikiwa nimekaa kwenye benchi alikuja nesi akaniambia niende chooni nikaoge na kubadilisha nguo. Kwa sababu sikujua, nikaenda,” alisema Asha. Alisema akiwa chooni anajiandaa kuoga, uchungu ulikata ghafla na baada ya dakika chache aliona kitu kinaning’inia sehemu za siri kisha kikadondoka chini. Baada ya kuona hivyo,...