Wanamgambo wa Kiislam wa kundi la Boko
Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria wametuhumiwa kushambulia shule
moja na kuwaua wanafunzi kadhaa.
Polisi nchini Nigeria wameliambia
Shirika la Habari la Uingereza, Reuters kwamba wote waliouawa ni
wavulana na kwamba baadhi ya miili ya wanafunzi hao imeungua na kubaki
majivu.(Hudugu)
Taarifa zinazohusianaMauaji, afrika magharibi
Taarifa ya jeshi la Nigeria imesema shambulio hilo limefanyika katika jimbo la Yobe.
Taarifa ya jeshi la Nigeria imesema shambulio hilo limefanyika katika jimbo la Yobe.
Wakaazi wa mji wa Buni Yadi katika jimbo hilo, wamesema washambuliaji hao walivamia usiku na kuwachinja baadhi ya wanafunzi.
Wamesema baadhi waliuawa kwa kupigwa risasi.
Walimu katika chuo cha serikali ya
shirikisho katika mji wa Buni Yadi wameliambia shirika la habari la AP
kwamba wanafunzi wapatao 40 waliuawa katika shambulio hilo ambalo
lilianza mapema Jumanne asubuhi.
Jeshi limethibitisha kwamba shambulio
hilo limetokea katika hosteli za wanafunzi lakini limesema haliwezi
kutoa taarifa zaidi kwa sasa.
Kundi la Boko Haram limekuwa
likishutumiwa kuendesha vitendo vya mauaji kaskazini mwa Nigeria,
yakiwemo mauaji ya mapema mwezi huu katika jimbo la Yobe.
Boko Haram, lina maana ya"Elimu ya
Magharibi ni dhambi" katika lugha ya Kihausa, mara kwa mara limekuwa
likishambulia shule katika siku za nyuma.
Watu kadhaa wameuawa katika
mashambulio mawili yaliyotokea wiki iliyopita. Katika tukio moja,
wanamgambo hao wa Boko Haram, waliteketeza kijiji kizima na kuwapiga
risasi wakaazi wa eneo hilo waliokuwa wakijaribu kutoroka
CHANZO BBC
Comments