IKIWA imepita miezi kadhaa tangu anaswe katika mtego wa kujiuza na
makachero wa OFM ya Global Publishers, staa wa Bongo, Baby Madaha
ametangaza kuachana na sanaa ya muziki na filamu kwa maelezo kuwa
amechoshwa na maisha ya presha. Akistorisha na paparazi wetu juzikati
jijini Dar es Salaam, Madaha alisema ishu ile imemsababishia matatizo
makubwa ya kifamilia na hata kibiashara, hivyo kujutia mchezo mzima
ulivyokuwa.
Alisema filamu anayoisambaza kwa sasa na kibao chake cha mwisho kukitoa
cha Mr. Dj ndizo zitakazofunga pazia la mambo ya sanaa kwa upande wake.
“Nimeamua kuachana na sanaa kabisa, siwezi kuishi maisha ya presha
yasiyo na uhuru. Nitarudi kwenye fani yangu niliyosomea (hakutaka
kutaja), maana naishi maisha ambayo hayana amani kabisa,” alisema.
Hivi karibuni Madaha aliingia kwenye kumi na nane za Oparesheni Fichua
Maovu ‘OFM’ ya Global Publishers ambapo alipatana bei ya kutoa uroda kwa
‘mfanyabiashara’ wa madini kutoka jijini Mwanza aliyejitambulisha kwa
jina la Mike – kumbe ulikuwa mtego.
Comments