Na Osman Mohamud, Mogadishu
Kadiri maguruneti ya kurushwa kwa mota na mashambulio ya ulipuaji wa
mabomu kifedhuli kumetisha wakaazi wa Mogadishu katika wiki za hivi
karibuni, utawala wa Benadir umekuwa ukiongeza jitihada za kutokomeza
uungaji mkono wa al-Shabaab kwa njia ya kujenga uelewa katika mji mkuu
huo.
Wanamgambo wa ndani wakipiga doria soko la
Hamar Weyne la Mogadishu tarehe 12 Februari, 2014. Utawala wa Benadir
unashiriki katika jitihada za kuboresha ushirikiano baina ya raia na
vikosi vya usalama katika mapigano dhidi ya al-Shabaab. [JM Lopez/AFP]
Utawala huo unatafuta kuboresha ushirikiano wa raia katika kupambana
dhidi ya al-Shabaab wakati wa kampeni ndefu ya mwezi mmoja ya kujenga
uelewa iliyozinduliwa tarehe 8 Februari. Programu hiyo inalenga kutoa
mafunzo kwa watu 200 kutoka kila idara ya wilaya kutimiza jukumu hilo
kwa kuwafikia umma katika vitongoji vyao na maeneo ya kazi.
Kama sehemu ya jitihada hizo, Gavana wa Benadir na meya wa Mogadishu
Mohamud Ahmed Nur wanapanga kutembelea kila wilaya huko Mogadishu,
wakitumia siku moja katika kila eneo kukutana na wakuu wa wilaya na
wakaazi wa eneo hilo.
Katika moja ya mkutano katika wilaya ya Hawl Wadag Jumanne (tarehe 11
Februari), Nur alizungumza kwa uwazi kauli nzito dhidi ya al-Shabaab
siku moja baada ya ulipuaji wa mabomu mawili katika mji mkuu huo
ukilenga maofisa wa serikali.
Meya wa Mogadishu Mohamud Ahmed Nur
(kulia) na mwimbaji wa Kisomali Hibo Nura wakiwa katika kampeni ya
kujenga uelewa kwenye jengo la Plaza la Jiji tarehe 27 Septemba, 2013,
ambapo walijadili hatari ya itikadi ya al-Shabaab. Nur anaendeleza
jitihada za kutokomeza itikadi ya al-Shabaab huko Mogadishu pamoja na
kampeni nyingine iliyozinduliwa Februari 2014. [Osman Mohamed/Sabahi]
"Ninashangaa kwa nini tunasikia kuwa wanachama wa al-Shabaab wanakamatwa
na [vikosi vya usalama]," Nur alisema. "Vikosi vya usalama vinapaswa
kuwatokomeza wakati huo huo na sababu yake ni kwa vile wamethibitisha
umwagaji damu ya raia , na watu wawapige mawe hadi kufa."
Comments