Na Julius Kithuure, Nairobi
Huku kesi dhidi ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kwenye Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai imeahirishwa kwa muda usiojulikana, watu wa
Kenya wanatoa maoni mbalimbali kuhusu mwelekeo na namna nzuri ya kuona
haki ikitendeka.
Mwandanamaji wa Kenya akiangalia picha za
vurugu za baada ya uchaguzi wakati wa maandamano huko Nairobi mwaka
2011. [Simon Maina/AFP]
Ingawa kuna maoni tofauti, karibia kila mmoja ana kitu cha kusema kuhusu
hili. Baadhi wanaunga mkono uahirishaji huo wa kesi hiyo, wakati
wengine wanasema waendeshaji kesi wa ICC wanapaswa kustahimili. Wengine
bado wanatoa wito kwa njia mbadala wa Kenya badala ya mahakama ya
kimataifa.
Kesi dhidi ya Kenyatta katika ICC imekuwa na vizuizi mbalimbali kutoka
ilipoanza, huku mashahidi mbalimbali wakiondoa ushahidi wao na madai
kuwa ushahidi umechafuliwa na pande zote za kesi. Katika mwezi wa
Disemba, Mwendesha Mashtaka wa ICC Fatou Bensouda alikiri kwamba hakuwa
na ushahidi wa kutosha kumshtaki Kenyatta kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu
wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 hadi 2008, na mnamo
tarehe 23 Januari timu ya waendesha mashtaka iliomba kuahirisha kesi
hiyo kwa muda usiojulikana.
Kenyatta ana masuala 'muhimu zaidi' ya kuzingatia
Wanaomuunga mkono Kenyatta wasema uendeshaji mashtaka unakosa ushahidi
mzito na kuondolewa kwa ushahidi muhimu kumedhoofisha kabisa kesi hiyo.
Picha iliyochukuliwa tarehe 8 Aprili,
2011, ikionyesha Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Uhuru
Kenyatta wa wakati huo (wa pili kushoto) kwenye Mahakama ya Kimataifa ya
Makosa ya Jinai. [AFP]
"Ni wazi kwamba sasa kesi dhidi ya raisi huyu ni yenye kasoro na yenye
kiasi kidogo cha uuaji," mbunge wa Juja Francis Munyua Waititu aliiambia
Sabahi. "Basi ni kwa nini rais apoteze nguvu zake, muda na rasilimali
kwa suala ambalo halina kichwa wala mkia?"
Comments