Gari la kuondoa theluji likiwa kazini huko Atlanta, Georgia
Dhoruba kali ya majira ya baridi kali imesababisha zaidi ya watu 300,000 eneo la kusini mashariki mwa Marekani kukosa umeme wakati dhoruba hiyo ikielekea eneo la kati ya Atlantic na sehemu za kaskazini mashariki mwa taifa hili.
Dhoruba imesababisha kunyesha kwa darzeni ya sentimeta za theluji kote katika eneo la Washington DC hapo Alhamis. Wakati katika baadhi ya maeneo ya Washington imeripotiwa kuwepo mpaka sentimeta 46 za theluji.
Serikali kuu imefungwa pamoja na
darzeni ya serikali za mji na mashule. Huko North na South Carolina,
dhoruba imesababisha barabara ndogo na barabara kuu hazipitiki na
kulazimisha madereva kuacha magari yao.
Watabiri wa hali ya hewa wamesema
Carolina zote mbili zilitarajiwa kupata zaidi ya sentimeta 20 za barafu
na theluji hadi Alhamis asubuhi baada ya kupata mchanganyiko wa theluji
na mvua hapo Jumatano.
Hali ya hewa imesababisha maelfu ya
safari za ndege kufutwa kwa muda, abiria kukwama kwenye viwanja vya
ndege. Darzeni ya vifo vimeripotiwa kusababishwa na dhoruba ikiwemo watu
watatu kufariki wakati gari la kubeba wagonjwa lilipoteleza kwenye
barabara zilizokuwa na barafu huko Texas.
CHANZO:VOA
Comments