Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kwamba mshambuliaji wa kimataifa wa Mexico anayekipiga Manchester United Javier Hernandez yupo mbioni kujiunga na kundi la wachezaji watakaondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huu.
Hernandez amekuwa akikosa nafasi ya kucheza mara nyingi katika kikosi cha David Moyes jambo lilalotajwa kumfanya akose raha ndani ya club.
Mmexico huyo mapema jana ali-retweet tweet ya Sky Sports iliyokuwa ikihusu yeye kujiunga na Tottenham msimu ujao ambapo baadae baada ya mchezo wa sare ya 2-2 vs Fulham ambao aliingia kipindi cha pili, Hernandez aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram kwamba: “Muda wa kuongea vitu vingi utakuja…..”
Comments