Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwakumbusha watu wote
wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT)
mwezi Novemba, 2014 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha
usajili kilichoanza rasmi tarehe 1 Januari, 2014 kwa ada ya Shilingi
50,000/=kwa wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT
kitaishia tarehe 28 Februari, 2014.
Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya
mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz. Kabla
ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya
mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na
kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au Mpesa.
Comments