Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha
Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua
watoto wanne mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia
Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa
anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na
watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa
kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na
watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.
Misaada kwaajili ya Aida Nakawala (25)
mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya mara baada
ya kufikishwa katika makao makuu ya Globu ya Jamii jijini Dar es salaam
baada ya kusafirishwa bure toka Uingereza na Wazee wa Kazi Serengeti
Freight.
Misaada ya hali na mali imeanza
kumiminika kwa ajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha
Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto
wanne mapacha kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa
2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.
Msamaria mwema wa Uingereza, Bi
Gladness Sariah, ametuma maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya
watoto, ambavyo vimewasili salama katika ofisi za Michuzi Media Group
(MMG) inayoendesha Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya
kusafirishwa bure na Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko
Uingereza.
Hivi sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa mama huyo, Mbeya Yetu Blog, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama Aida mizigo yake haraka iwezekanavyo.
Kwa niaba
ya mzazi wa mapacha hao, Michuzi Blog na Mbeya Blog zinatoa shukrani za
dhati kwa msamaria mwema Gladness Sariah kwa wema na upendo
aliouelekeza kwa mzazi huyo. Huo ni mfano wa kuigwa, na tunatarajia
misaada zaidi itatolewa na wasamaria wema ambao tunajua mko wengi kila
kona ya dunia.
Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com
nasi tutafikisha ubani wako. Serengeti Freight wametoa ofa ya kusafirisha bure misaada ya aina hii ASANTENI SANA
Michuzi Blog/Mbeya Yetu Blog
CHANZO:MTA KWA MTAA
|
Comments