Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini sheria mpya inayotoa
adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu uchi au kuhusika
na vitendo vinavyohusisha picha zenye watu uchi.
Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi fupi sana au 'Mini Skirt'
kama zinavyojulikana au blausi ambazo zinaonyesha kifua chao hadharani
na kusababisha hisia za kingono .
Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika
kwa ajili ya mafunzo au wakati wa michezo na hafla za kitamaduni.
Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kapmala, waziri wa maadili na
utawala bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa Rais Museveni
alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili bada ya bunge
kuipitisha.
Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati dhidi ya vitendo hivyo itabuniwa ili
iweze kutekeleza sheria hiyo kwa kuhakikisha kuwa picha, au video zenye
watu uchi zinanaswa na kuharibiwa.
Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka katika sekta mbali mbali ikiwemo ya habari na utumbuizaji.
Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote atakayepatikana akijihusisha na
vitendo cya watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi , kuona sinema za watu
wakiwa uchi au kuchapisha picha za watu walio uchi kwa lengo la kuleta
hisia tofauti utachukuliwa hatua kali za kisheria.
Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu.
Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia visivyo watafungwa hadi miak
10 na wale watakaopatiokana na hatia ya kuhusisha watoto katika
biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.
Comments