Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika (Misca) katika kata ya Boy-rabe, makao makuu ya wanamgambo wa anti-balaka, mjini Bangui, februari 19 mwaka 2014 ... FRED DUFOUR/AFP |
Na RFI
Milio ya risase za rashasha na miripuko ra roketi na gruneti imesikika
mapema leo asubuhi karibu na uwanja wa ndege wa mjini Bangui, ambako
waandamanaji wameweka vizuizi dhidi ya vikosi vya kimataifa, ameshudia
muandishi wa AFP.
Risase zimerushwa hadi karibu na kambi ya wanajeshi wa Ufaransa
wanaolinda eneo moja la uwanja wa ndege, na wako tayari kujibu
mashambulizi yoyote dhidi yao, milio hiyo ya risase imesababisha watu
kua na hofu katika maeneo jirani ya uwanja wa ndege.
Duru za kijeshi zinafahamisha kwamba milio hio inashukiwa kwamba huenda
ni ufyatulianaji risae kati ya wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika
(Misca) na wanamgambo wa kundi la wa kristo la anti-balaka wanaoishi
karibu na maeneo jirani na uwanja wa ndege.
Mamia ya watu wanaoishi katika kambi kubwa ya wakimbaizi wa ndani iliyo
karibu na uwanja wa ndege, wamekimbilia sehemu ndege zinaegesha baada ya
kutua, lakini wanajeshi wa Ufaransa wameingilia kati na kuomba watu hao
kurejea kambini.
Makundi madogo madogo ya watu, ambao wamekua wakiandamana wakipinga
operesheni ya wanajeshi wa Ufaransa dhidi ya wanamgambo wa kundi la
ant-balaka, wameweka vizuizi kwenye barabara inayoelekea kwenye uwanja
wa ndege.
Kwenye umbali wa mita zaidi ya mia moja na ua wa uwanja wa ndege, vijana
kati ya 200 na 300wamekua wakipaza sauti wakilani operesheni (Sangaris)
inayoendeshwa na wanajeshi wa Ufaransa na ile ya wanajeshi wa kikosi
cha Umoja wa Afrika (Misca) pamoja na siasa ya viongozi wa srikali ya
mpito.
Milio ya risase imesikika pia jana usiku hadi mapema leo asubuhi katika
kata ya Boy-Rabe, makao makuu ya wanamgambo wa anti-balaka, na katika
eneo la kaskazini mwa mji.
Moja kati ya mpango wa rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ni
kuhakikisha usalama umerejea nchini, na alahidi kuanzisha vita dhidi ya
wanamgambo wa kundi la anti-balaka.
Mapigano hayo mapya yamesababisha ujumbe wa viongozi wa ngazi ya juu wa
Umoja wa Mataifa wanahirisha ziara ambayo wangeifanya leo jumatano
katika mji wa Bossangoa ( kilomita 250 kaskazini magharibi na mji wa
Bangui).
Via kiswahili.rfi.fr
Comments