Mkurugenzi wa Tanzania House Of Talent (T.H.T) Bw. Ruge Mutahaba amemtaka Mkurugenzi wa Deiwaka Production Bw. Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu amwombe msamaha dhidi ya tuhuma zilizotolewa juu yake kuhusiana na kampeni ya Malaria No More.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo mchana Mikocheni jijini Dar,Ruge Mutahaba amesema kuwa amempa Mr II masaa 72 ili aweze kumuomba msamaha/radhi dhidi ya shutuma ambazo amezisambaza dhidi yake kuhusiana na sakata hilo la Malaria No More .
"Kiukweli nimeamua kuwaita waandishi wa habari ili niweke sawa haya mambo, mimi nilipewa tenda na kampuni ya Roundtrip kusimamia upande wa wasanii, jukwaa pamoja na`kusimamia mambo mengine hilo ndiyo lilikuwa jukumu langu mimi kama mimi,haya mambo mengine yanazungumzwa juu yangu sijui yanatoka wapi,hivyo namuomba Mr II aniombe radhi/msamaha kwa vyombo vile vile vya habari alivyovitumia kunidhalilisha mimi na kunivunjia uaminifu kwa jamii ninayoiongoza".Alisema Ruge Mutahaba.
Comments