Waziri Mkuu Zimbabwe Margan Tsvangirai amewataka wawekezaji kurudi kuwekeza katika nchi yake kutokana na uwepo wa amani katika nchi hiyo.Waziri Tsvangirai amesema Serikali yake imefanya kilajitiada kufanya mazungumzo ya mezani na vyama vya upinzani nchini humo ili kurudisha hali ya amani.
Bwana Tsvangirai alisema hali ya uchumi nchini humo iliporomoka kwa kasi kutokana na vurugu za uchaguzi uliopita hali iliyopelekea wawekezaji kuhamisha vitegauchumi vyao.Pia amezitaka jumuiya za kimataifa kuiondolea vikwazo nchi ya Zimbabwe kwani kwa kufanya hivo uchumi utakuwa kwa kasi na kusaidia vijana wengi kupata ajira kwa wawekezaji wapya.Hata hivyo Bwana Tsvangirai amesema imefika wakati kwa Waafrika kuweza kusimama yenyewe kwa kushirikiana kwa pamoja ili iweze kunufaika na rasilimali zake.
Alisema mkutano wa kujadili hali ya uchumi wa Afrika ni wakati muafaka wa kubadilishana mawazo ya jinsi mataifa ya magharibi yanatumia njia gani katika kuendeleza maendeleo ya mataifa yaoAkizungumzia Serilkali ya mseto katika nchi yake Bwana Tsvangirai alisema hali ya malumbano ni ya kawaida katika nchi yoyote duniani na anaamini umoja wa Serikali yao utafika mbali na upo kwa ajili ya manufaa ya Wazimbabwe.
Waziri Tsvangirai alisema kwasasa nchi ya Zimbabwe inanafasi nyingi za uwekezaji akitolea mfano sekta ya Kilimo na ambapo imekuwa ni tegemeo kubwa katika uchumi wa taifa hilo na kusema kuwa hali ya kisiasa kwa sasa ni shwari.
Bwana Tsvangirai alisema kuna marekebisho kadhaa ambayo Serikali yao inayafanya ambapo aliyataja baadhi ya kurekebisha sheria mbalimbali mfano sheria ya vyombo vya habari ambayo itawapa uhuru zaidi wanahabari ili kuwe na uchaguzi wa haki.

Comments