Julius Tindwa ambaye ni Kocha wa Manyara akipokea jezi kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Arusha (ARFA) Khalifa Mgonja katika makabidhiano yaliyofanyika jana, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha. Wengine kulia ni Soud Abdi, Mjumbe wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), katikati ni Adam Brown, Katibu wa ARFA, kulia kabisa ni Goodluck Kway, Ofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wadhamini wa Kili Taifa Cup kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Moh amed Shein,alipokuwa akifanya mahojiano na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupitia ZBC TV na kutoa wito kwa Watanzania hasa wa Zanzibar kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji vitambulisho hivyo,ambapo zoezi hilo linatarajia kuwanza Oktoba 15 mwaka. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu mjini Zanzibar leo,(kulia) Mtangazji wa ZBC TV Nasra Nassor. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu
Comments