Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Dar es SalaamWafanyakazi katika ngazi ya utumishi wa umma wametakiwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuboresha huduma ya utendaji kazi na hatimaye kufikia malengo ya utoaji haki kwa wananchi wote na kwa wakati muafaka.
Akisoma hotuba kwa niaba ya mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema wakati akifungua mkutano wa wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliofanyika Dar es Salaam leo, amewaambia wafanyakazi hao kuwa juhudi na maarifa katika kazi ndio silaha muhimu katika kutekeleza majukumu ya utendaji kazi.
“Ili tuweze kupata mafanikio ni wazi kwamba kada zote za utumishi wa ndani ya ofisi hii zinapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ili kuleta tija na ufanisi katika sehemu zetu za kazi,” Amesema Jaji Werema.
Jaji Werema ameliambia baraza hilo kuwa lina wajibu wa kutambua na kujadili vipaumbele vya Ofisi hiyo ili kuhakikisha kwamba fedha zinatengwa kwa majukumu na madhumuni ya kuboresha huduma na kuondoa kero za wananchi kwa ujumla.
“Wajumbe wa baraza la wafanyakazi mnapaswa kutoa miongozo na ushauri katika matumizi bora ya fedha zilizopangwa kwa kuzingatia vipaumbele pamoja na kutatua matatizo yanayojitokeza katika utekelezaji wa mambo yaliyo ndani ya uwezo wenu”, Ameongeza Jaji Werema.
Akizungumzia suala zima la uchaguzi, Jaji Werema amelikumbusha baraza hilo kuwa katika mwaka huu wa uchaguzi, Ofisi yake ina jukumu kubwa la kusimamia maandalizi ya uchaguzi, uchaguzi wenyewe na kesi zitakazotokea baada ya uchaguzi hivyo amelitaka baraza hilo kufanya kazi kwa bidii ili kufanikisha zoezi hilo la uchaguzi.
Jaji Werema amefafanua kuwa shughuli za uchaguzi zitaathiri bajeti ya Serikali kutokana na fedha nyingi kuelekezwa kwenye uchaguzi hali itakayosababisha Serikali kupunguza mgao wa fedha katika taasisi zake, hivyo amewataka wafanyakazi hao kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ili kutekeleza majukumu ya msingi yanayotakiwa.
Aidha Werema ametoa wito kwa wafanyakazi hao kuyapa umuhimu masuala ya jinsia na ukimwi pamoja na kuepuka kuwanyanyapaa waathirika ili kuwafanya waishi maisha malefu na yenye furaha katika jamii na sehemu zao kazi.

Comments