Matukio ya uharamia ya utekeji nyara wa meli bahari ya Hindi karibu na Tanzania, unaofanywa na maharamia wa Kisomali, yanazidi kupamba moto, baada ya ile meli ya Uingereza kuwatimua wiki iliyopita, na meli nyingine kuvamiwa majuzi, leo meli ya Mafuta ya Ufaransa imevamiwa.
Balozi wa Ufaransa atazungumza na Waandishi wa habari kesho Saa 6:30 mchana hapa Umoja House huku akisindikizwa na mabalozi wa Uingereza, Ujerumani, Uholanzi na Jumuiya ya Ulaya.
Comments