Afisa habari wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Frolian Kaijage ameongea na vyombo vya habari leo
na kusema kwamba tiketi za kombe la dunia kwa watanzania walionunua zimeshawasili ambapo shirikisho la
mpira wa miguu duniani FIFA limetuma tiketi 380 ambazo zilinunuliwa
na watanzania.
Akionyesha tiketi hizo kwa waandishi wa habari , Kaijage a limesema kwa wale walionunua
tiketi hizo wanatakiwa kwenda kuchukua wakiwa na risiti ili waweze kupatiwa tiketi hizo
na baada ya kupatiwa tiketi hizo ili kupata viza katika ubalozi wa Afrika Kusini wanatakiwa
kwenda na Tiketi ya ndege, tiketi ya kuingilia mpirani, Paspoti ya kusafiria pamoja na picha
moja itakayotumika kwa utambulisho wa mhusika kwa usalama zaidi na taarifa mbalimbali wakati
yuko katika fainali hizo endapo kutatokea lolote akiwa nchini Afrika Kusini
Wakati huohuo Rais wa Shirikisho hilo la TFF Reodger Tenga amesema bado wako kwenye mazungumzo
na timu ya taifa ya Brazil ili iweze kuja hapa nchini kwa mchezo mmoja wa kirafiki na mara mambo
yatakapokuwa sawa TFF itatoa taarifa zaidi juu ya ujio wa timu hiyo.
Comments