Skip to main content

Bw.Donald Kaberuka Achaguliwa Tena Rais wa Benki


Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika leo tarehe 27 mwezi mei hapa Abidjan

imemchagua tena Bw.Donald Kaberuka kuwa Rais wa Benki hiyo kwa kipindi cha pili. Bw.

Kaberuka alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Rais wa Benki hiyo mwaka 2005.


Kuchaguliwa kwake kwa kipindi cha pili kumetokana na mafanikio makubwa ambayo ameyaleta

katika benki hiyo na kuleta maendeleo katika taasisi hiyo muhimu ya kifedha na kwa bara la

Afrika. Hii ilibainika kutoka kwa Magavana waliotaka Rais huyo kuendelea na wadhifa wake.


Katika kukubali kuthibitishwa kwake katika cheo hicho. Bw Kaberuka aliwashukuru Magavana hao

kwa kuwa na imani na uongozi wake katika benki. “Nina farijika sana kuona kuwa ninyi

Magavana mna imani kubwa na mimi hadi kunichagua tena ili niweze kuiongoza taasisi hii

muhimu, kwa kweli nina shukuru sana”,alisema.


" Ningependa kutoa shukrani zangu za pekee kwa uongozi na wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo

ya Afrika kwani wao ndio wamenifikisha hapa kwani mimi ni Rubani tu. Alisema Kaberuka baada

ya kuthibitishwa katika nafasi hiyo.


“Nilichaguliwa kwa mara ya kwanza miaka mitano iliyopita.Benki imeongezeka mara mbili .

Lakini katika kipindi cha miaka mitano ijayo, tutajikusanya na kuiweka Afrika katika kiwango

cha juu kimataifa",alieleza.


"Tutajitahidi kuhakikisha kuwa tunafikia mategemeo ya watu wa Afrika. Tutafanya kazi

ilitufikie lile lengo la kuwa na bara moja linaloshirikiana kwa kila kitu, tutapambana na

mabadiliko ya hali ya hewa na kuhakikisha kuwa tunakuwa na chakula cha kutosha, alisema.


Kikosi cha Benki ya Maendeleo ya Afrika kimekuwa na maendeleo makubwa katika shughuli zake

za ndani na uongozi, vilevile imelenga zaidi uwajibikaji katika kuleta maendeleo Afrika hasa

katika kukuza sekta binafsi, kufadhili miradi inayoshughulikia miundo mbinu, na kusisitiza

kuwepo biashara ya pamoja katika kukuza uchumi wa bara la Afrika.


Katika ripoti iliyotoka hivi karibuni inayohusu muonekano wa Uchumi katika Bara la Afrika

inasema kuwa, ifikapo mwaka 2011 uchumi utakuwa kwa asilimia 5.2 tofauti na kiwango cha sasa

cha asilimia 4.5 kwa mwaka 2010.


Kwa sababu ya kuongezeka kwa mahitaji ya Benki ya maendeleo ya Afrika Benki imekuwa na uhaba

wa fedha uliosababishwa na mtikisiko wa uchumi. Kwa sababu hiyo basi Magavana pia wametoa

uhalalisho wa kuongeza mtaji kwa taasisi zake kwa asilimia 200% hii itasaidia kuendesha

miradi na programu ambazo nchi wanachama imezipanga.


Chini ya uongozi wa Bw. Kaberuka Benki imejitahidi kuhakikisha kuwa kunakuwa na mawasiliano

ya karibu kati ya nchi zilizoko kwenye ukanda mmoja na sekta binafsi. Aidha benki

imefanikiwa kuwa na ofisi katika kila nchi barani Afrika.Magavana waliainisha.
Bw. Kaberuka, ambaye ni Rais wa saba wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, aliapishwa tarehe 1

mwezi septemba mwaka 2005 kwa mara ya kwanza huko Tunisia.


Kabla ya kujiunga na Benki, Bw. Kaberuka alikuwa Waziri wa fedha na mipango ya Uchumi wa

Rwanda kuanzia mwaka 1997 mpaka 2005, na alitambulika kama Mkuu aliyejenga upya nchi ya

Randa ambayo ilikuwa na vita na aliweza kuijenga nchi hiyo kwa kuweka programu nzuri

zilizoleta mabadiliko ya uchumi.


Alianzisha na kuendeleza maboresho katika uongozi na uchumi mkuu katika mambo ya fedha,

mambo ya mabenki, bajeti, miundo muhimu ya nchi ikiwa ni pamoja na benki kuu ya nchi iliyo

huru. Na matokeo ya maboresho hayo ni kukua kwa uchumi wa Rwanda ulio imara na kuiwezesha

nchi hiyo kufaidika kwa kufutiwa madeni yake mwezi Aprili mwaka 2005.


Bw. Kaberuka anauzoefu wa zaidi ya miaka 12 katika mambo ya Benki, katika mambo ya fedha na

biashara, katika mambo ya biashara ya vitu kimataifa na katika maendeleo ya sekta kabla

yakujiunga na serikali.


Akiwa Waziri wa Fedha na mipango kiuchumi, Rais huyu wa Benki ya maendeleo ya Afrika

alitumika kama Gavana wa Benki ya Dunia kwa Rwanda, vilevile katika shirika la fedha la

kimataifa na Benki ya Maendeleo ya Afrika.


Alisoma Tanzania hadi kidato cha sita na kupata shahada ya kwanza katika chuo kikuu cha Dar

es salaam. Vilevile alisoma Uingereza ambapo alipata shahada ya uzamili katika filosofia ya

Uchumi na uzamifu katika filosofia ya Uchumi huko chuo kikuu cha Glasgow - Scotland.
Bw. Kaberuka anazungumza vizuri sana Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili.
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu- Wizara ya fedha na Uchumi
Abidjan.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...