Waziri wa Mambo ya Ndani Rawlence Masha
Na Mohammed Mhina na Seni Jilulu, wa Jeshi la Polisi DAR ES SALAAM
Wafanyakazi Raia wa Wizara ya Mambo ya Ndani wamesema hawatahusika na mgomo na kwamba wanaunga mkono kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kuvitaka vyama vya wafanyakazi nchini kuendelea na mazungunzo na Serikali kupitia upya madai yao.
Kauli hiyo imetolewa na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi vya wizara hiyo wakati wakizungumza kwenye mkutano uliotishwa na Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani Bw.Mubarack Abdullwakil, Mwenyekiti wa TUGHE Wizara ya Wambo ya Ndani Idara ya Polisi Bw.Alcado Nchinga amesema kimsingi wanaunga mkono kauli ya raisi ya kuendelea na mazunguzo ili kufikia muafaka ambao utaleta tija katika taifa.
Bw.Nchinga amesema wao kama vyombo vya kulinda usalama hawatangia katika mgomo kwani wasingependa kuona damu inamwagika kupitia mikononi mwao na wameahidi kulinda amani iliyopo hapa nchini kwa nguvu zote kwa manufaa ya watanzania wote. “Lazima tusikilize kauli ya Mh.Rais kwani ameahidi kushughulikia matatizo ya wafanyakazi.”Alisema Bw. Nchinga na kuongeza kuwa Wafanyakazi wote wa Wizara ya Mambo ya ndani kwa lengo la kumuunga mkono Mh.Rais Kikwete.
Kwa upande wake Katibu wa TUGHE Wizara ya Mambo ya Ndani Bw. Simon Isack Mjelu amesema madai yao ya msingi watandelea kudai ikiwa ni pamojana kupunguziwa kodi katika mishahara na kuongezwa mshahara ili kuendana na hali ya uchumi. Bw.Mjelu amesema hawaoni kwanini wagome na kusisitiza kuwa “muda wa ukifika tutajulishana hapa kwa kuomba ruhusa kwa katibu mkuu na kuwajulisha wanachama wote na kusisitiza kuwa tunaheshimu kauli ya Mh.raisi”.
Kwa upande wake Katibu wa TUGHE wa watumishi Raia wa Jeshi Polisi nchini Bw. Dolnad Lonungu, wamesema hawaungi mkono mgomo ama maandamano kwa vile wao ni viongozi waliopo ndani ya wizara nyeti kitaifa. Naye Mkurugenzi wa Idara ya Malalamiko Wizara ya Mambo ya Ndani BW.Augustine Shio amehoji “sisi nani kukataa amri ya rais” hivyo akasisitiza wafanya kazi wote kummunga mkono mh.
raisi na kukubaliana na kuendelea na majadiliano na serikali kwa kuwa serikali ni sikivu itashughulikia madai ya watumishi wake.
Naye Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi anayesimamia wafanyakazi Raia DCP Nevin Mashayo, amesema kauli ya raisi imeonyesha ukweli kwamba TUCTA walikubaliana na majadiliano na serikali hivyo amewataka wafanyakazi wote kufika kazini na kuedelea na majukumu yao kwa taifa.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Mambo ya ndani Bw.
Mubarack Abdullwakil, amewahimiza wafanyakazi wote wa wizara hiyo kuwahi kazini licha ya kwamba baadhi ya barabara zitafungwa kufuatia kutumika kwa wajumbe wa mkutano wa EWF.

Comments