MSANII mahiri wa muziki wa Hip Hop nchini , Kalama Masoud ‘Kalapina’ ametangaza kuwania udiwani katika mojawapo ya kata zilizopo wilayani Kinondoni katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam, Kalapina ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Kikosi cha Mizinga la Kinondoni jijini Dar es Salaam, alisema kuwa, anapenda sana siasa na ipo kwenye damu yake, ndiyo maana nyimbo zake nyingi amezielekeza kwa jamii.
Aidha Kalapina maarufu kwa jina la ‘Pina’ alisema kuwa, lengo lake jingine la kuwania nafasi hiyo ni kuwasaidia wakazi wa kata hiyo atakayogombea, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiongozwa na viongozi wanaojinufaisha wenyewe pasipo kuangalia maslahi ya wapiga kura wao.
“Unajua ni muda mrefu viongozi wanaoiongoza kata ile wamekuwa na propoganda zisizokuwa maana yoyote, matokeo yake wananchi wamekuwa wakiteseka kila siku, sasa lengo langu ni kuleta mapindizi ya kweli katika kata ile,” alisema.
Alisema kwa hivi sasa ni mapema mno kuitangaza kata atakayowania kwa kile alichodai kuwa anaweza akaanza kuwekewa mizengwe na wanasiasa wengine ambao tayari wameshanza kumuofia baada kutangaza azma yake.
Wasanii mblimbali katika uchaguzi mkuu ujao wanatarajiwa kugombea nafasi mbali za uongozi baada ya kupewa kipaumbele cha kufanya hivyo na Raisi Kikwete.

Comments