Skip to main content

VODACOM SASA KUCHONGA NI KARIBU NA BURE


Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akiongea na wanahabari wakati wa uzinduzi wa huduma ya Habari ndiyo hii ya kuongea kwa shilingi 1 kwa sekunde hivi karibuni.HIVI karibuni Vodacom Tanzania imezindua huduma ya Cheka Time ambapo mteja atatumia robo shilingi kwa sekunde. Hii ni huduma ya aina yake na hajawahi kutokea katika historia ya mawasiliano hapa nchini.Kwa mantiki hiyo, Vodacom hivi sasa ndio imekuwa kampuni ya simu za mkononi ambayo inatoa huduma kwa gharama nafuu ukilinganisha na kampuni nyingine nchini ambazo Watanzania walio wengi wanazimudu.Vodacom hivi karibuni pia ilizindua huduma ya HABARI NDIYO HII kwa lengo la kurahisisha mawasiliano kweye familia yake na kwamba kupitia huduma hii wateja wa Vodacom wanaweza kupiga simu kwa kiwango cha shilingi moja kwa sekunde kwa masaa 20 kwa siku.Huduma hii ni Vodacom kwenda Vodacom pekee.Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba amesema kwamba wateja wa Vodacom kupitia CHEKA TIME kwa wale wanaojisajili kwa shilingi 200 na shilingi 500 sasa wanaweza kuongea kwa chini ya robo shilingi kwa sekunde, sawa na senti 0.22 kwa sekunde.“Hii inamaanisha kwamba Vodacom sasa ndiyo mtandao unatoa huduma kwa gharama rahisi kuliko mitandao mengine yote nchini”, amesema.Kwa mujibu wa Bi Makamba, huduma hii itaiwezesha familia ya Vodacom kuwasiliana kwa gharama ya chini zaidi na kwamba ana imani kwamba huduma hii itachochea ukuaji wa uchumi wetu kwa maana ya Watanzania wenye shughuli mbalimbali wana uhakika wa kuwasiliana bila kikwazo chochote.Anafafanua kwamba mbali na huduma hii viwango vingine vya CHEKA TIME ya shilingi 2000 na 5000 bado vinaendelea kutumika kama kawaida.Bi Makamba amesema kwamba huduma ya Vodajamaa nayo inaendela kama kawaida, ambayo ni mojawapo ya njia inayoiwezesha familia ya Vodacom yenye watu zaidi ya milioni saba (7) kuwasiliana kwa gharama nafuu kwa dakika na mteja anaweza kusajili watu watano kwa mara moja na watu 15 kwa mwezi mmoja.Huduma ya hii inamaanisha kwamba zaidi ya wateja milioni saba wa kampuni ya simu ya Vodacom nchini watanufaika na huduma hii mpya ya ‘HABARI NDIYO HII’ itakayokuwa endelevu na sio ya kipindi maalumi”, amesema.Kiwango hiki cha malipo kwa watumiaji wa simu wa Vodacom Tanzania ni muendelezo wa utoaji wa huduma na promosheni zinazoambatana na zawadi mbalimbali ambazo huwafanya watumiaji wake kuwasiliana kwa urahisi.Bi Makamba ana matumaini kwamba mabadiliko ni hakika, kuanzishwa kwake kutaboresha sekta ya mawasiliano nchini na kuwapa fursa wateja kuongea zaidi na zaidi na hivyo kuchochea shughuli mbalimbali za maendeleo kwani mawasiliano ya uhakika ni injini ya maendeleo.“Wengi wanadhani ni jambo lisilowezekana kwamba Vodacom, ambayo inachukuliwa kuwa inatoza huduma zake kwa gharama za viwango vya juu sokoni, kuamua kutoa huduma zake kwa gharama za chini na kuweza kuendeleza nyingine”, amesema.“Vodacom Tanzania inachukua fursa hii kuwashukuru wateja wake na Watanzania wote na kuwaahidi kuendelea kutoa huduma na kuleta bidhaa zilizokuwa na ubora wa hali ya juu. Vodacom imekuwa ikitoa huduma za simu kwa muda wa miaka kumi sasa na inatarajia kukua zaidi katika sekta ya mawasiliano kwa mwaka huu na miaka ijayo”, ameongeza.Bi Makamba alifafanua kwamba Vodacom ina shauku kubwa kwa kutoa huduma hii iliyokuwa rahisi na ya bei ya chini katika soko la wakati huu kuliko kampuni nyingine zote za simu hapa nchini.Huduma hizi za Vodacom pia ni muafaka kabisa kwa wanavikundi mbalimbali vya uzalishaji mali, wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati, wakulima, wanafunzi,wafanyakazi pamoja na wanafamilia.Kuhusu huduma nyingine kama M-PESA amesema kampuni yake inawashukuru wateja wake zaidi ya milioni mbili ambao wamesjisajili na huduma hii.Amesema hii ni hatua muhimu lakini pia kwa mwaka huu kuna mambo mengi mazuri, mathalani kupitia huduma ya M-PESA wateja wa Vodacom kwa kutumia simu zao za mkononi hivi sasa wanaweza kulipia ankara za Umeme, maji na DSTV bila kupanga foleni lakini pia kupata huduma kwenye maduka makubwa.Wateja wa Vodacom wanaunganishwa na Vodafone M-PESA, huduma inayotolewa kwa ushirikiano na kundi la Makampuni ya Vodafone.Ametoa mfano wa Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya Dawasco, imeanzisha huduma ya bure ya kulipia maji, ambapo wateja wa Vodacom Tanzania sasa wanaweza kulipia ankara zao za maji kwa kupitia simu zao za mkononi kupitia huduma ya Vodafone M-PESA.

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

LEO NI BUNGE LA BAJETI

Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo. -WANANCHI WATAKA IPUNGUZE UKALI WA MAISHA MACHO na masikio ya mamilioni ya Watanzania na wadau wa nje, leo yanaelekezwa Dodoma ambako Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12 itasomwa.Wananchi wengi wamekuwa na shauku ya kujua mwelekeo wa bajeti hiyo hasa katika kipindi hiki ambacho wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei vyakula na bidhaa za mafuta. Kwa takriban wiki nzima iliyopita, baadhi ya wananchi wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu katika vyombo vya habari, wakiisihi serikali kuhakikisha kuwa bajeti ya mwaka huu inawaondoa katika hali ngumu ya maisha. Bajeti hiyo itakayosomwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo itatangazwa kwa wakati mmoja na bajeti za serikali za nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika mtazamo wa kuimarisha mshimakano na umoja wa nchi hizo. Kwa kawaida na mazoea ya muda mrefu, baj...