Piacha na habari Francis Dande.
Mwenyekiti wa Chama Cha Jamii (CCJ), Mh. Richard Kiyabo leo jioni ameugua ghafla na kukimbizwa katika kituo hicho kutokana na maumivu ya shingo pamoja na kifua kubanana Francis Dandewa Globu ya JamiiHALI ya afya ya Mwenyekiti wa Chama cha Jamii (CCJ), Mh. Richard Kiyabo imebadilika ghafla na kukimbizwa katika kituo cha Afya cha Dk. Hameer kilichopo maeneo ya Faya jijini Dar leo.
Akizungumzika hali yake huku akiwa kitandani Mwenyekiti huyo alisema kuwa afya yake ilianza kudhohofika leo na kukimbizwa katika kituo hicho majira ya saa tisa alasiri kutokana na kupata maumivu makali ya shingo pamoja na kifua kubana.
Aidha alisema kuwa hali hiyo inatokana na kuvamiwa na watu wanne majira ya saa tatu asubuhi na kisha kumkaba shingo na kumpora mkoba wake uliokuwa na kiasi cha sh. laki tano, Laptop pamoja na reja iliyokuwa na orodha ya majina ya wanachama wa chama hicho kwa upande wa Zanzibar.
Alisema kuwa kabla ya tukio la uporaji halijafanyika watu hao walimtisha na kisha kumtolea vitambulisho vilivyokuwa vikionyesha kuwa ni wafanyakazi wa Idara ya Usalama wa taifa. “Niliwaaambia kuwa kama nina makosa wanipeleka katika vyombo vya sheria lakini walizidi kunikaba”.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa tukio hilo analihusisha na hujuma za kisiasa kutokana na mazingira yake na kuliomba jeshi la polisi kulinda raia wake na kufanya uchunguzi wa kina kujua waliohusika na tukio hilo ili sheria ifuate mkondo wake.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mwenyekiti huyo alisema kuwa: "Hata kama nikifa leo watanzania wasimtafute katika makaburi yaliyopakwa rangi nzuri ila wamtafute kwenye mioyo ya watanzania wanyonge milioni 40 walio mijini na vijijini, hali si nzuri sina hela hata mchana sijala,” alisema Mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa watanzania wamchangie katika gharama za matibabu ambazo ni kubwa.
Daktari wa zamu Dk. Sombi Charles aliyekuwa akisaidiana na Dk. Nassor alisema kuwa katika kumfanyia uchunguzi wao walibaini kuwepo kwa matatizo katika shingo na kifua kutokana na kupata mgandamizo wa kitu chenye ncha butu kwenye shingo na kumsababishia matitizo katika mishipa ya fahamu.
“Hivi sasa tumempatia matibabu ya awali ili kupunguza maumivu aliyokuwa nayo wakati tukimsubiri mtaalamu wa mishipa ya fahamu (aliyemtaja kwa jina moja la Dk. Othman) afike ili kumfanyia uchunguzi wa kina ili kutoa tiba sahihi kwa mgonjwa.

Comments