Tsunami ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM mkoani Morogoro imeiacha CHADEMA
taaban wilayani Gairo baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Mkalama
wilayani Gairo Zefania Magiga na wenzake 68 kutangaza kuhamia CCM,
wakati wa mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Aprili 17, 2013, kwenye Uwanja
wa shule ya Msingi, Umoja mjini Kilosa mkoani Morogoro.(Picha na Bashir
Nkoromo).
Tsunami ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM mkoani Morogoro imeiacha CHADEMA
taaban wilayani Gairo baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Mkalama
wilayani Gairo Zefania Magiga na wenzake 68 kutangaza kuhamia CCM,
wakati wa mkutano wa hadhara.
Magiga na wenzake wamekabidhi kadi zao za Chadema kwa Kinana, na kupewa
kadi za CCM, baada ya kutangaza kukihama chama chao na kujiunga na CCM
kwenye mkutano huo ambao ulifurika mamia ya wananchi, kwenye Uwanja wa
shule ya Msingi Gairo B, katika wilaya mpya ya Gairo.
Mbali na kupokea wanachama hao kutoka Chadema, kwenye mkutano huo,
Kinana alipokea wanachama wapya 120, waliojunga na CCM na kufanya jumla
ya wanachama wapya waliojinga na CCM kwenye mkutano huo kuwa 188.
Comments