Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa, wa pili kulia, akifafanua jambo kwa Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbawara, Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung. Mpango huo unalenga kuwawezesha wateja wa CRDB nchini kujipatia simu za Samsung Galax S3,Samsung Galax note2 na Samsung Galax note 10 katika duka lolote la Vodacom na kuzilipia kwa awamu kwa kati ya miezi 12 na 24. Kulia ni Meneja wa huduma za kibenki wa CRDB, Farida Mbwana.
Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbawara akimsikiliza Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa, wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango wa ushirikiano baina ya Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Benki ya CRDB PCL na Samsung. Mpango huo unalenga kuwawezesha wateja wa CRDB nchini kujipatia simu za Samsung Galax S3,Samsung Galax note2 na Samsung Galax note 10 katika duka lolote la Vodacom na kuzilipia kwa awamu kwa kati ya miezi 12 na 24,kushoto ni Mkuu wa Vifaa vya Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Bw.Mgopelinyi Kiwanga.
Comments