MPIGA gitaa la bass wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', Jojo Jumanne amefunguka na kutamba kuwa yeye ni mmoja wa wasanii wakongwe nchini, kwani ameanza muziki tangu akiwa kijana mdogo.
Jojo ambaye amejipatia umaarufu kupitia kipaji chake cha kupiga gita la bass, amekuwa na kawaida ya kupagawisha mashabiki mara kwa mara kwa kupiga gitaa lake kwa umahiri.
"Nina miaka kumi na tatu ndani ya Twanga Pepeta na sijawahi kufikiria kuhama bendi tangu nijikite rasmi na ninaona wanamuziki wanaohamahama, bendi zao hizo ni mbwembwe zao tu," alisema.

Jojo alielezea hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni Jumamosi iliyopita ambaye alielezea mafanikio yake ya msingi katika
maisha.
Alisema moja ya mafanikio yake akiwa na bendi hiyo ni pamoja na kumiliki viwanja vitatu jijini Dar es Salaam, ambapo kimoja anakifyatulia matofali kwa ajili ya ujenzi.
Alifafanua pia kuhusu kuchelewa kumiliki nyumba, ambapo alisema huenda kuishi kwake kwenye nyumba ya urithi kumechangia.
"Kwa sasa bado ninaishi kwenye nyumba ya urithi maeneo Victoria Kinondoni, labda hali hiyo pia imechangia mimi kubweteka kwa kukaa kwenye nyumba hiyo, kwani
silipi kodi ya nyumba hapa mjini ndiyo maana naona ujenzi wangu umekuwa wa kusuasua," alisema Jojo.
Comments