AMENESA! Ndiyo kauli rahisi, ambayo unaweza kuitumia baada ya mwanamuziki mkongwe Jennifer Lopez 'JLo', kutoa picha inayomuonesha akiwa na Chris Brown.
Picha hiyo imetolewa katika ukurasa wa mtandao wa jamii wa Twitter, ambapo inamuonesha mwanamama huyo akiwa amejilaza begani kwa Brown, huku pembeni yao kukiwa na mtu mwingine.
Picha hiyo imezua majadiliano kwa sasa nchini humo kutokana na tabia ya JLo, kupenda kubadili wavulana hasa wale ambao amewazidi umri, huku Brown pia akiwa hajatulia.
Lakini Lopez mwenyewe amedai picha hiyo alipiga na Brown anayetamba na wimbo wa Don't Wake Me Up, katika studio ya mtayarishaji Cory Rooney.
Pia mtayarishaji huyo ndiye anayeoongoza kwa kutengenezea nyimbo zaidi ya 30 za JLo, kwa sasa bado kumekuwa na maswali kuhusu wawili hao kwamba wapo kwa ajili ya kazi au kuna jambo linaendelea nyuma ya pazia.
Comments