Wakwaza kutoka kushoto ni Bosco Seti na wakatikani ni Lufingo na wa mwisho ni Mzee Chillo
FILAMU ya Mkataba, ambayo awali iliyosababisha kupotea funguo za gari aina ya Toyota Hiace ya marehemu Steven
Kanumba, na kuleta 'kizazaa' tayari imekamilika.
Funguo hizo zilipotea wakati mdogo wake Kanumba, Bosket Seti alipokuwa akishiriki katika kurekodi filamu hiyo saa
6 usiku maeneo ya Kiwalani, Dar es Salaam.
Ujio wa filamu hiyo ya Mkataba, ambayo ilianza kurekodiwa Februari 18, mwaka huu ilizua kizazaa kwa ndugu wa
marehemu Kanumba waliposikia kwamba funguo za gari hilo zimepotea.
"Ilikuwa majira ya usiku, tukiwa katika kazi ya uchukuaji wa picha ya filamu ya Mkataba, maeneo ya Kiwalani
mara baada ya kumaliza kazi hiyo, Seti alitaka kuondoka ndipo alipogundua kuwa ameangusha fungu hizo.
"Tulijaribu kuutafuta ufunguo huo, bila mafanikio hali ambayo ilitulazimu kulala mpaka asubuhi ndani ya
gari hilo ili kulichunga lisije likaibiwa," alisema Lufingo.
Alisema ilipofika asubuhi walilazimika tene kuutafuta ufunguo huo, bahati nzuri wakaupata.
Filamu ya Mkataba, inatarajiwa kuingia sokoni muda wowote kunzia sasa mara baada ya kukamilika.
Lufingo pia alishacheza
filamu nyingine kama Kisanduku, ambayo ndiyo ya kwanza kwake, pamoja na Pesa haramu ikiwa ya pili na ya
tatu ndiyo hii ya Mkataba, aliyowashirikisha wasanii wengine Dude, Mzee Jengua na Mzee Chillo.

Comments