Na Adnan Hussein, Mogadishu
Serikali ya shirikisho ya Somalia imeunda na kukipa mafunzo kikosi
maalumu cha askari kufanya operesheni dhidi ya ugaidi huko Mogadishu na
kuzuia mipango ya al-Shabaab ya kulipua mabomu ya kujitoa muhanga kwa
siku zijazo.
Askari wa Jeshi la Taifa la Somalia
wakitembea wakati wa gwaride la jeshi tarehe 14 Aprili huko Mogadishu.
Serikali ya shirikisho inaandaa kikosi maalum imara 1,000 waliopewa
mafunzo kwa ajili ya operesheni dhidi ya ugaidi kusambazwa katika mji
mkuu huo. [Na Stuart Price/AU-UN IST PHOTO/AFP]
Serikali inapanga kusambaza kikosi imara 1,000 ifikapo mwishoni mwa
Aprili, kitakachojumuisha vikosi kutoka matawi kadhaa ya vikosi vya
jeshi na vikosi vya usalama kwa mujibu wa Mohamud Ahmed Hirsi, meneja
katika idara ya ugavi na usafirishaji wa watu na vitu wa Jeshi la Ulinzi
la Somalia.
Kikosi hiki kitabomoa na kuharibu ngome za ugaidi na maficho, kuondoa
kabisa operesheni zao na kutegua mabomu, katika jitihada za kurejesha
amani na kanuni katika mji mkuu.
"Vikosi hivi vinawajibika kutafuta magaidi na wale wanaotuhumiwa
kujihusisha katika operesheni za uuaji kwa sababu za kisiasa dhidi ya
wahamasishaji amani, waandishi wa habari, polisi na maofisa wa jeshi,"
Hirsi aliiambia Sabahi. "Miongoni mwa malengo yake ni kushambulia
vikundi vya kigaidi ambavyo vinafanya mauaji, wizi na kuiba mapato,
pamoja na kuingilia mali binafsi, taasisi za serikali na migahawa."
Askari wa Jeshi la Taifa la Somalia
wakishiriki katika mazoezi ya mafunzo tarehe 28 Machi katika kambi ya
mafunzo ya Jazeera huko Mogadishu, mahali ambapo wakufunzi wa Misheni ya
Umoja wa Afrika nchini Somalia wanaendesha vikosi vya Somalia kwa njia
ya upangaji mpana wa ufundishaji askari na mbinu za kijeshi. [Na Tobin
Jones/AU-UN IST PHOTO/AFP]
Baadhi ya vikosi kutoka katika kikosi kipya vitafanya doria kwenye
maeneo ya mji ambako waasi wamejulikana kujificha, vikitekeleza hatua
kali za ulinzi, Hirsi alisema.
Vikosi vingine vitalinda usalama wa vituo vya ukaguzi vya kando ya
barabara mahali pengine popote katika mji mkuu wakiwataka waendesha
magari na pikipiki kuonyesha vitambulisho na kukabidhi magari yao kwa
ukaguzi wa usalama.
Comments