NYOTA wa muziki nchni Marekani Ray J , anatarajia kuanzisha vuguvugu kubwa
baa ya kuingia studio na kutoka na ngoma itakayoitwa ‘I hit it first’
ambapo kunatetesi kuwa itakuwa imemlenga moja kwa moja Kim Kardashian
mpenzi wa mkali wa Hip Hop Kanye West.
Mtandao mmoja wa kijamii nchini humo,umemuelezea Ra J ,pamoja na kimwana Kim Kardashian waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi karibu miaka 10 iliyopita, mpaka kufikia hatua ya kurekodi video ya ngono ambayo baada ya kuachana, Ray J aliitupia kwenye mtandao na kupata
faida kubwa kwa kujiingizia mkwanja mrefu tu.
Pia mtandao wa TMZ , umemuelezea msanii Ray J kuwa tayari ameanza mipango ya kutengeneza
ngoma ya ya video model ambaye anafanana kabisa na Kardashian.
Comments