Kituo cha TV maarufu nchini Kenya, Citizen TV kiliipiga marufuku kuicheza video ya ngoma mpya ya P-Unit, 'You Guy'.
Video hiyo iliyoongozwa na Clarence Peters inaonesha wanawake warembo wakicheza ambao ndio sababu ya marufuku hiyo.Katika maelezo yake, Citizen iliandika:
"the video is too explicit for prime TV airing and while the show targets youthful adults, there is evidently a very young audience too due to the fact that it is an interesting show that also shows during hours when most working adults are not even home to watch any TV"
Vera Sidika a.k.a Vee Beiby
Utafiti uliofanywa kutazama ni mrembo gani video Queen wa Kenya alieandikwa sana kwenye internet toka video mpya ya P Unit ya You Guy itoke, umeonyesha kwamba model huyu aliecheza kwenye hiyo video Vera Sidika a.k.a Vee Beiby ndio ameandikwa sana kwa zaidi ya stori 120 kwenye internet.
Nakumbuka siku chache tu baada ya hiyo video kutoka, taarifa zilisambaa kutoka Kenya kwamba video hiyo imefungiwa kurushwa kwenye kituo cha Citizen Tv kutokana na ukali wa picha, hasa za huyu mrembo.Kimeeleza chanzo kimoja nchini hapa.
Comments