Mafanikio yenye mvuto kwa wasanii wa Vichekesho Bongo kutoka kwa WILL SMITH ambaye ni mme wa JADA PINKETT SMITH .
Will Smith ambaye alizaliwa September 25, 1968, ambaye aliwahi kuwa muigizaji wa
kipindi cha The fresh Prince ,akiwa mchekeshaji mbali na fani hiyo alikuwa
pia rapper mwenye mvuto maarufu sana nchini marekani.
kipindi cha The fresh Prince ,akiwa mchekeshaji mbali na fani hiyo alikuwa
pia rapper mwenye mvuto maarufu sana nchini marekani.
Mnamo mwaka 1992 alimuoa Sheree Zampino walifanikiwa kupata mtoto mmoja Trey
Smith ambaye ni mcheza Basket maarufu nchini marekani. Wadau mtakuwa mnajua vema
inshu hii kwani jamaa aliachana na Sheree mnamo mwaka 1995.
Na baadaye alifanikiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na na kuhamua kuoana na Jada
Pinket mnamo mwaka 1997 na katika ndoa yao wamefanikiwa
kupata watoto wawili ambao ni Jaden Smith na Willow Smith ambao nao wanachanja
mbuga katika fani walizorithi kwa wazazi wao.
Jaden Smith amezaliwa July 8, 1998 ni mcheza filamu mzuri tuu anayechipukia na
filamu alocheza ni ''karate kid'' wadau mnaohusudu fani ya ucheshi , kama
utaikumbuka mdau au kama hujaiona itafute .
Ni kati ya sinema nzuri sana akiwa sambamba na Jackie Chan.
Willow Smith alizaliwa October 31, 2000 ,mwenye umri wa miaka 11 hadi mnamo mwezi
wa 10/2012 anatimiza 12, ameonesha kipaji chake cha kuimba na ni mwanamuziki
anayechipukia ambae alishatoa ngoma ikapokelewa poa sana, na ata hapa Bongo
ilipokelewa poa ikiitwa jina la ''whip my hair''na pia amewahi
kushiriki katika filamuinaitwa ''I Am Legend''.
Kiukweli Wadau wengi kuanzia huko barani America na Duniani kote kwa ujumla wanaizimia
sana familia hii , ni mfano wa kuigwa huko marekani
na hata hapa kwetu, nawatakia maisha bomba na marefu pia.
Hata hapa nchini Tanzania taswira ya wasanii wa vichekesho ilianza kupata
mtazamo chanya , baada ya kundi maarufu la Ze Commedy kuonesha kufikia
mafanikio mengine tofauti na mtazamo hasi wa hapo awali tasnia ya vichekesho
ilikuwa aijafikirika kama wanaweza kuwa watu wenye kupata heshima kama
walivyoanza kupewa heshima kubwa ya mtazamo chanya mfano wa kundi la
Zecommedy ambalo lionaonesha kuwa nuru ya mafanikio kwa wachekeshaji wachanga
kupata mvuto wa kufikia mafanikio kwa siku za usoni.
Comments