Korea Kaskazini kuwaondowa wafanyakazi wake 53,000 katika eneo la viwanda la pamoja na Korea Kusini la Kaesong na kusitisha shughuli zote za kibishara katika kituo hicho kutokana na kile ilichokiita uchochezi wa kivita.
Kim Yang-Gon afisa mwandamizi wa chama tawala nchini Korea Kaskazini
amekaririwa akisema katika taarifa kwamba Korea Kaskazini itawaondowa
wafanyakzi wake wote katika kanda hiyo na wakati huo huo kusitisha kwa
muda shuguli zinazofanyika hapo na kuangalia iwapo iruhusu kuwepo kwa
kituo hicho au ikifungilie mbali.
Kim ambaye alitembelea kituo hicho cha viwanda cha Kaesong leo asubuhi
amesema wamelazimika kuchukuwa hatua hiyo kutokana na uchochezi wa
kivita unaotaka kuifanya Kaesong kuwa mahala pa malumbano kutokana na
kuongezeka kwa hali ya wasi wasi wa kijeshi katika Rasi ya
Korea.Ameongeza kusema kwamba hali itakavyokuwa huko mbele itategemea
mwenendo wa serikali ya Korea Kusini.
Wafanyakazi wa Korea Kusini wapigwa marufuku
Korea Kaskazini imewapiga marufuku mameneja wa Korea Kusini na
wafanyakazi wake kuvuka mpaka na kuingia katika kituo hicho cha viwanda
kilioko kilomita 10 ndani ya ardhi ya Korea Kaskazini tokea Jumatano.
Comments