Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amesema
Zanzibar ni nchi ya biashara hivyo inataka kujitegemea iweze kupunguza
ushuru ili wananchi wapate kununua bidhaa kwa bei nafuu.
Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF
Maalim Seif Sharif Hamadi akiwahutubia wananchi wa Mkwajuni katika mkuto
wa hadhara wa chama hicho uliofanyaka katika viwanja vya mpira
Mkwajuni, April 06/2013
Kauli hiyo ameitoa huko katika viwanja vya Skuli ya Mkwajuni Wilaya ya
kaskazini “A” wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa huo.
Amesema iwapo Zanzibar itapata mamlaka yake kamili itaweza kuwa na bandari huru, ushuru na bei za bidha vitapungua.
“Zanzibar ni nchi ya biashara tunataka tuwe na bandari huru ili tupate
kuweka kodi ndogo na ushuru ukipungua bei za bidhaa zitapungua”alieleza
Maalim.
Aidha amesema kuwa wananchi wanataka kuwepo kwa bandari na kupungua
ushuru ili wapate kuweka bei wanazotaka wenyewe na sio kuamuliwa na mtu
mwengine.
Akizungumzia Muungano Maalim Seif amesema wazanzibari waliowengi
wanataka serikali ya mkataba iwe na mamlaka kamili na isiingiliwe katika
maamuzi yake.
Comments