Na Bosire Boniface, Garissa
Wakati Kenya inaanza kujiondoa katika utawala wa serikali kuu, magavana
watatu kutoka kaskazini mashariki wanasema wanapanga kupunguza mivutano
miongoni mwa koo kwa kutumia sera sawa ya ajira kwa kazi za utumishi wa
umma.
Viongozi kadhaa wa jimbo wanasema kuwa
watatumia mfumo wa kiasi ambacho kila kundi linapaswa kupata ili kujaza
nafasi za utumishi wa umma. Juu, Wananchi wa Kenya wakisubiri katika
foleni mjini Nairobi. [Na Will Boase/AFP]
"Serikali shirikishi ni muhimu katika kuondoa wimbi la vurugu za
kikabila ambazo zimezuia maendeleo katika mkoa huo," alisema Ali Ibrahim
Roba, gavana mpya mteule wa Kata ya Mandera.
Roba alisema atajaribu kubadilisha tabia iliyoshikiliwa muda mrefu
ambapo viongozi wa mkoa waliwapendelea watu wa koo zao kwa nafasi za
utumishi wa umma katika tawala zao. Zoezi kama hilo huwatenga watu
kutoka koo nyingine, jambo linalosababisha kuzuka kwa upinzani wa
vurugu, alisema.
"Sasa, tutaongozwa na katiba ambayo inaelezea kuwa jimbo linapaswa
kuzizingatia jamii zote na makundi mahsusi katika kuajiri na kugawana
rasilimali," aliiambia Sabahi, na kuelezea kuwa Kata ya Mandera ina koo
tatu kuu na kiasi cha koo saba ndogondogo.
Comments