KWENYE miti hakuna wajenzi! Ndivyo unavyoweza kusema kwa sasa, kutokana na kitendo cha msanii Justine Beiber, kuendelea kuziba masikio kwa mpenzi wake Selena Gomez.
Hivi karibuni, Selena alitoa kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Come and Get It, ambacho amemaanisha kuwa njoo na ukichukue.
Wimbo huo kwa sasa umetokea kuwa gumzo kutokana na mashairi yaliyopo ndani yake, ambapo msanii huyo bado anaendelea kulilia penzi la Beiber.
Katika utoaji tuzo wa MTV Movie, Selena alionekana kuvutia wengi kutokana na jinsi alivyopendeza baada ya kupiga picha, zilisikika kelele za 'Come and get it'.
Comments