Mpaka sasa watu watatu wameshakufa
kutokana na mashambulio ya mabomu mawili yaliyoripuka wakati wa mbio
ndefu za marathon katika mji wa Boston nchini Marekani
Mabomu mawili yaliripuka kwenye mitaa iliyokuwa imejaa watu karibu na
sehemu ya kumalizia mbio za marathon. Watu wasiopungua watatu wamekufa
kutokana na miripuko ya mabomu hayo yaliyoutikisa mji wa Boston katika
jimbo la Marekani la Massachusettes.
Jee ni magaidi tena?
Watu wengine zaidi ya140 walijeruhiwa katika kadhia ya umwagikaji wa
damu. Vioo vilivunjika na sehemu za miili ya binadamu ilitapakaa- hali
iliyosababisha wasiwasi kwamba magaidi wameishambulia tena Marekani.
Msemaji wa Ikulu ya Marekani ambae hakutaka kutajwa kwa sababu uchunguzi
bado unaendelea, ameeleza kuwa mashambulio hayo yanazingatiwa kuwa ni
kazi ya magaidi.
Akitoa tamko juu ya mashambulio hayo Rais Obama aliepuka kutumia neno
gaidi, alieleza kwamba maafisa wa Marekani hawajui ni nani aliyeyatega
mabomu hayo na kwa nini.
Hata hivyo afisa mmoja wa Ikulu ya Marekani alisema baadae kuwa miripuko
hiyo iliyotokea kwenye mbio za marathoni zenye jadi ya miaka mingi,
inazingatiwa kuwa kitendo cha ugaidi.
Obama asema aliefanya mashambulio atapatikana:
Comments