Na Victor Melkizedeck Abuso
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametoa agizo la kupunguza mamlaka ya
naibu wake Riek Machar hatua ambayo huenda ikasababisha machafuko ya
kikabila nchini humo.
Salva Kiir rais wa Sudan Kusini
Hatua hiyo ya rais Kiir inaamanisha kuwa Machar ambaye ni mpiganaji wa
zamani wa msituni na anayefahamika kuwa na ushawishi mkubwa ndani ya
kabila la Nuer sasa atahusika tu na kazi aliyopangiwa kikatiba nchini
humo, lakini haikufahamika wazi ni mamlaka yepi hayo yaliondolewa.
Kuanzia siku ya Jumanne, jukumu kubwa la Machar litakuwa ni kumwakilisha
rais Kirr wakati anapokuwa nje ya nchi hiyo kuwa mwanachama wa baraza
la Mawaziri na baraza la Kitaifa la Usalama.
Uamuzi wa rais Kiir pia una maana kuwa hatua za Machar za kujaribu
kuweka mipango ya kuliunganisha taifa hilo ambalo limekumbwa na ukabila
huenda zikadidimia.
Kamati ya uwiano wa kitaifa nchini humo imevunjwa na rais Kiir suala
ambalo raia nchini humo wamesema wameshangazwa na hatua hiyo ya rais.
Comments