KLABU ya Yanga inatarajia kuandaa hafla ya kuchangisha michango kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wake mpya wa kisasa maeneo ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam. Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zimeeleza kuwa, mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Kikwete. Kwa mujibu wa habari hizo, uamuzi wa kuandaa hafla hiyo ulifikiwa katika kikao cha kamati ya utendaji ya klabu hiyo kilichofanyika hivi karibuni mjini Dar es Salaam. "Kamati ya utendaji iliyokutana hivi karibuni ilikubaliana kuandaa hafla kubwa ya kuchangisha mamilioni ya pesa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo,"alisema mmoja wa viongozi wa kamati hiyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini. Mbali ya kuandaa hafla hiyo, kamati hiyo imeshapendekeza ramani ya uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, ambao ujenzi wake unatarajiwa kugharimu dola milioni 50 za Marekani Chanzo hicho cha habari kilieleza kuwa, uwanja huo ndio chaguo la kwan...