Skip to main content

WATEJA WANAOTUMIA HUDUMA YA M-PESA SASA KUTUMIA ATM ZA DTB KUTOLEA FEDHA



Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati (kushoto) akiwaelezea waandishi wa habari jinsi ya kutoa fedha  kwenye mashine za kutolea fedha za DTB kupitia huduma ya Vodacom M PESA ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote walipo nchini.  Huduma hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.…
Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati (kushoto) akiwaelezea waandishi wa habari jinsi ya kutoa fedha  kwenye mashine za kutolea fedha za DTB kupitia huduma ya Vodacom M PESA ambapo sasa wateja wanaotumia huduma hiyo wanaweza kutoa pesa kupitia mashine hizo popote walipo nchini.  Huduma hiyo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.
Meneja  Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, akitoa fedha kwa mara ya kwanza baada ya kuzinduliwa kwa huduma ya kutoa fedha kupitia mashine za kutoa fedha za DTB kupitia huduma ya M PESA. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati.
Salum Mwalim na Sylvester Bahati wakifurahi baada ya kutoa fedha kwa mara ya kwanza kupitia mashine za kutoa fedha za DTB kwa huduma ya M PESA.
Dar es Salaam, 26th Machi, 2013 ...Ukuaji wa teknolojia ya huduma maarufu ya kutuma, kupokea fedha pamoja na kufanya malipo ya huduma mbalimbali kwa njia ya simu za mkononi ya kampuni ya Vodacom ya M-pesa inazidi kupanuka na hivyo kuongeza kiwango cha matumizi ya huduma hiyo kuzidi kuboresha maisha na kuyafanya kuwa rahisi zaidi.

Katika kufikia mafanikio hayo Benki ya Diamond Trust (DTB) leo imetangaza ubia wa kibiashara na kampuni ya Vodacom Tanzania ubia ambao unawawezesha wateja wa M-pesa kuwa na uwezo wa kutoa fedha kutoka katika akuanti za M-pesa kwa kutumia mashine za kutolea fedha (ATM) za benki ya Diamond Trust.

Wakitangaza na kuzindua huduma hiyo jijini Dar es salaam Mkuu wa Kitengo za Uzalishaji na Masoko wa DTB, Sylvester Bahati,  amesema hayo ni mafanikio mengine ya kibishara kwa benki hiyo ya DTB katika kupanua wigo wa huduma na namna benki hiyo inavyoweza kuunganisha teknolojia ili kuleta urahisi kwa watanzania.

“DTB inayo Furaha kubwa kuwa sehemu ya mapinduzi ya kiteknolojia hapa nchini. Hii ni huduma ya kwanza na ya aina yake ambayo hakuna shaka kwamba inaashiria uwezo wa DTB katika kuleta ufumbuzi wa namna bora ya kutumia teknolojia kurahisisha maisha.”Amesema Bahati

“Tukishirikiana na Vodacom tunawawezesha wateja wa M-pesa walio karibu na benki zetu na hususan mtandao wa ATM kuwa na uhakika wa kutoa fedha kutoka akaunti zao za M-pesa saa ishirini na nne katika siku zote saba za wiki.”

Bahati amesema jambo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki sanjari na kuboresha hali ya maisha na uchumi kwa watanzania wote mijini na vijijini.

Hata hivyo hii ni frusa ya kipekee kwa wateja wa benki ya DTB ambao wamejiandikisha kwa ajili ya huduma ya M-Pesa hawana haja tena ya kutembelea matawi ya benki hiyo ili kuweza kuweka amana zao au kuhamisha fedha kwa biashara, marafiki na familia zao. Pia uzinduzi wa huduma hiyo utawezesha kujenga urahisi wa kuruhusu wasiotumia huduma ya benki kupata huduma za kifedha karibu nao.

Azma ya DTB ni kuzidi kuongeza kasi na maboresho ya utoaji wa huduma kwa wateja wake na washirika wake wengine kwa kuhakikisha inaendelea kupanua wigo wa huduma zake ikiwemo kuongeza ATMs, matawi na huduma nyinginezo kwa lengo la kusogeza karibu huduma za kibenki nchi nzima.

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa M- Biashara wa Vodacom Jacques Voogt, amesema, "Hii ni hatua nyingine ambayo tunaifikia leo. Kampuni ya Vodacom inaendelea kupanua mtandao wake wa huduma ya M-Pesa.”
Voogtz ameongeza kuwa ubia huo ni mwendelezo wa azma ya kampuni ya Vodacom kutumia fursa za teknolojia ya M-pesa kuzidi kuleta amsiha ya watu mikononi mwao kutumia simu za kiganjani.

“Wateja wa Vodacom M-pesa wanayo sababu nyingine ya kujivunia kuwa sehemu ya mtandao mpana wa huduma hii salama, rahisi na yenye kuaminika zaidi nchini wakiunganishwa na makampuni na hata tasisi zaidi ya 200 kufanya malipo ya huduma na manunuzi kwa urahisi na wepesi zaidi kupitia simu za viganjani.”Aliongeza Voogtz

Kuhusu DTB…..
Kuhusu Vodacom Tanzania:

Kampuni ya Vodacom Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na jamii katika shughuli za maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation. Vodacom Foundation ina nguzo kuu tatu: Afya, Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi sasa taasisi hiyo imechangia zaidi ya miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha, imeshinda tuzo mbalimbali za kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika kwa Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion Award ambayo hutolewa na kampuni mama ya Vodafone.
Vodacom Tanzania Limited ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania inayotumia teknolojia ya kisasa ya mawasiliano. Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty) Limited, South Afritca, ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited inamiliki hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na asilimia 35 zilizobaki zinammilikiwa na Mirambo Ltd.

Vodacom Tanzania imetangazwa kuwa Super Brand (Chapa Bora Zaidi) kwa miaka mitatu mfululizo, kutoka 2009 -2011.

Kwa mawasiliano:
Matina G. Nkurlu
Meneja Mahusiano
Vodacom Tanzania Limited.
Mlimani City Jengo namba 1. Ghorofa ya kwanza.
Simu namba: 0754 710 099
Email:mnkurlu@vodacom.co.tz
Kwa taarifa zaidi kuhusu kazi za Vodafone Foundation, Tembelea.
http://www.vodafone.com/content/index/about/foundation.html 

Comments

Popular posts from this blog

Thousands of protesters clash with police in Chicago: Chaos in the Windy City as 45 activists arrested and one cop stabbed after demonstrators target NATO

By DAILY MAIL REPORTER Thousands of demonstrators upset with the war in Afghanistan, climate change and the erosion of union rights have raised the intensity of a march in downtown Chicago on Sunday as world leaders assembled for a NATO summit. The protest, one of the city's largest in years, turned violent at the end of an anti-NATO march, where demonstrators confronted Chicago police, pushing against a line of officers several blocks from the lakefront convention center where President Obama hosted a gathering of world leaders. Authorities were seen making arrests one by one and leading individual demonstrators away in handcuffs. After a clash near McCormick Place, Chicago Police Superintendent Garry McCarthy said at a news conference that the protests resulted in 45 people being arrested and four officers suffering injuries - one from a stab wound in the leg. Scroll down for video Clash: Demonstrators try to flee the police as they are move in on them ...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Mwana muziki Marufu kwa jina la Chuck Brown Afariki Dunia Akiwa na umri wa miaka 75

View Photo Gallery — Chuck Brown dies at 75: The “godfather of go-go” has died By Chris Richards, Updated: Wednesday, May 16, 4:42 PM Chuck Brown, the gravelly voiced bandleader who capitalized on funk’s percussive pulse to create go-go, the genre of music that has soundtracked life in black Washington for more than three decades, died May 16 at the Johns Hopkins University hospital in Baltimore. He was 75. The death, from complications from sepsis, was confirmed by his manager, Tom Goldfogle. Mr. Brown had been hospitalized for pneumonia. Known as the “Godfather of Go-Go,” the performer, singer, guitarist and songwriter developed his commanding brand of funk in the mid-1970s to compete with the dominance of disco. Like a DJ blending records, Mr. Brown used nonstop percussion to stitch songs together and keep the crowd on the dance floor, resulting in marathon performances that went deep into the night. Mr. Brown said the style got its name because “the music j...