Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (Kulia) akizungumza na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa dawati la maswala ya Afrika katika Idara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Wang Heming (kushoto) baada ya kuwasili leo Machi 11, 2013 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhu, kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku kumi nchini China. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai). (Picha na Bashir Nkoromo).
………………………………………..
NA BASHIR NKOROMO, CHINA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amewasili leo Machi 11, 2013 nchini China kuanza ziara ya kikazi ya siku kumi, kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China.
Kinana ambaye ni ziara yake ya kwanza kufanya nchi za nje tangu ateuliwe kuwa Katibu Mkuu wa C CCM, Oktoba mwaka jana, amewasili akiambatana na ujumbe wa watu 14 wakiwemo viongozi na maofisa wa Chama na kupokewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Guangzhu, na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa dawati la maswala ya Afrika katika Idara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Wang Heming.
Comments