Mahakama ya ICC wanatarajiwa kuwa na kikao kutathmini athari ya kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta.
Mjini The Hague Uholanzi leo alasiri mahakama ya ICC inatarajiwa kufanya
kikao maalum kilichoitishwa na majaji kutathimini athari zinazoweza
kuonekana katika kesi dhidi ya Uhuru Kenyatta ambaye ni mmoja kati ya
watuhumiwa wa kesi ya ghasia za baada ya uchaguzi wa kenya mwaka 2007,
baada ya mwendesha mashataka mkuu wa mahakama hiyo wiki iliyopita
kutangaza uamuzi wa kuibwaga kesi dhidi ya mtuhumiwa mwengine katika
kesi hiyo aliyekuwa mtumishi wa umma Francis Muthaura.
Leo mawakili wa rais mteule wa Kenya Uhuru Kenyatta wanategema kuitia
msukumo pia mahakama hiyo kuitupilia mbali kesi dhidi ya mteja wao. Hata
hivyo kumekuwa na maswali mengi juu ya jinsi mahaka hiyo inavyoiendesha
kesi hiyo,hasa kutokana na suala la ushahidi katika upande wa mwendesha
mashataka wa mahakama hiyo.
Nimezungumza na mwanasehria wa Kimataifa kutoka London Gordon Mwikira
juu ya suala hili na kwanza anatoa tathmini yake juu ya kesi hiyo
ilivyo. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni
hapo chini.
Comments