Nachukua... nawekaa... waaaa! Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na mgombea
urais, Uhuru Kenyatta akipiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura
cha eneo la Gatundu nchini humo leo Machi 4, 2013. Wakenya walipopiga
kura leo katika uchaguzi mkuu kumpata rais mpya atakayerithi nafasi
inayoachwa na Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake na hadi sasa, ushindani
mkali upo baina ya Uhuru na Raila Odinga. (Picha: Reuters)
Safari hii piga ua lazima nishinde...! Waziri Mkuu wa Kenya na mgombea
urais kupitia Coalition for Reforms and Democracy (CORD), Raila Odinga
akipiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura cha Kibera, Nairobi
nchini humo leo Machi 4, 2013. Wakenya wanaendelea kupiga kura leo
katika uchaguzi mkuu kumpata rais mpya atakayerithi nafasi inayoachwa na
Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake na hadi sasa, ushindani mkali
unaonekana kuwapo kati ya Odinga na Uhuru Kenyatta. (Picha: Reuters)
Odinga akijaindaa kupiga kura yake kwenye kituo cha kupigia kura cha
Kibera, Nairobi nchini humo leo Machi 4, 2013. Wakenya wanaendelea
kupiga kura leo katika uchaguzi mkuu kumpata rais mpya atakayerithi
nafasi inayoachwa na Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake na hadi sasa,
ushindani mkali unaonekana kuwapo kati ya Odinga na Uhuru Kenyatta.
(Picha: Reuters)
Uhuru akiendelea na mchakato wa kumchagua mbunge wa Gatundu leo Machi 4,
2013. Wakenya walipopiga kura leo katika uchaguzi mkuu kumpata rais
mpya atakayerithi nafasi inayoachwa na Mwai Kibaki aliyemaliza muda wake
na hadi sasa, ushindani mkali upo baina ya Uhuru na Raila Odinga.
(Picha: Reuters)
Wananchi wa Kenya wakipanga foleni kupiga kura katika jiji la Nairobi, jana Machi 4, 2013.
Shoto-kulia-shoto- kulia...! Askari akisimamia foleni wakati wananchi wa
Isiolo nchini Kenya wakiendelea kupiga kura kumchagua rais mpya wa
Kenya jana Machi 4, 2013.
Hapa ni ahdi kieleweke...! Wananchi wa Kenya wakiwa katika foleni ndefu
kuhakikisha kuwa wanapiga kura kumchagua rais wao jana Machi 4, 2013
Comments