Wagombea wa uraisi nchini Kenya
Wakati harakati za kampeni za uchaguzi wa uraisi zinafikia ukingoni
nchini Kenya, Marekani imewataka raia wa Kenya kufanya uchaguzi wa amani
ili kumpata kiongozi mpya kwa amani.
Akizungumza kwa niaba ya serikali naibu msemaji wa serikali ya Marekani
Patrick Ventrell ameongeza kuwa Kenya inapita katika kipindi cha muhimu
na kihistoria na hivyo kuwasihi wagombea kuhakikisha wanaepuka kuwa
sababisho la umwagaji damu kama uliowahi kutokea katika uchaguzi wa
mwaka 2007.
Hata hivyo hali ya mvutano imeongezeka ambapo serikali ya Marekani
imewataka wakenya kutumia fursa hiyo kudumisha ukomavu wa demokrasia na
kutekeleza matakwa ya katiba mpya.
Msemaji huyo amesema kuwa ni matarajio ya wengi kuwa wakenya hawatajali
jinsi,kabila,dini,eneo analotoka mgombea ili kuchagua bali bali
watamchagua kiongozi bora kulingana na sifa stahiki.
Takribani raia elfu moja walipoteza maisha huku laki sita wakiyakimbia
makazi yao katika machafuko yaliyotokea katika kipindi cha uchaguzi wa
mwaka 2007.
Via kiswahili.rfi
Comments