Na: Albert Sanga, Iringa.
Mwaka 2001 nilihudhuria kongamano la kidini ambalo pamoja na mambo mengine lilijadili hali ya maendeleo ya Afrika. Kongamano hilo lilifanyika katika shule ya sekondari ya Bihawana iliyopo nje kidogo ya mji wa Dodoma. Mada iliyowasilishwa kuhusu Afrika ilikua na kichwa, "Je, Afrika imelaaniwa?".Mtoa mada mkuu alikua ni mzungu mmoja (mmishenari), ambaye aliamsha mjadala mkali kweli kweli mara baada ya kumaliza kuwasilisha hoja zake. Katika mjadala uliofuatia (baada ya mtoa hoja kumaliza) kulijitokeza makundi mawili baina ya wanakongamano; moja likisema na kuamini kua Afrika imelaaniwa na jingine likipinga kabisa laana ya Afrika. Upande uliokua ukisema Afrika imelaaniwa ulikua na hoja zenye nguvu kweli kweli na ulionekana kuuzidi ule upande uliopinga laana ya Afrika. Mmoja wa wachangiaji alisimama na kusema maneno yafuatayo, "Ndugu zangu mimi nawathibitishia kua Afrika tumelaaniwa na uthibitisho huu tunaupata kutoka kwenye Biblia katika Kumbukumbu la Torati 28: 15- 40. Biblia inasema kuwa...
Comments