Kiongozi wa Ujumbe wa Iran kwenye Mazungumzo ya Nuklia Saeed Jalili
Na Lizzy Anneth Masinga
Iran na mataifa yenye nguvu duniani wamemaliza Mazungumzo ya siku mbili
hapo jana nchini Kazakhstani na kukubaliana kufanya mazungumzo mengine
majuma kadhaa yajayo mazungumzo yatakayolenga Mradi wa nuklia wa Iran.
Iran imekana shutma kuwa imekuwa ikirutubisha madini ya Uranium kwa
kiasi kikubwa na kwa kasi kubwa ili kutengeneza Silaha za Nuklia, shutma
ambazo zimekuwa zikitolewa hasa na Israel na Mshirika wake mkubwa,
Marekani.
Awali suala hili lilijadiliwa katika Mazungumzo kwa awamu tatu katika
kipindi cha mwaka mmoja pekee, huku Mkutano wa mwisho uliofanyika mwezi
June ulimalizika bila kukubaliana kukutana tena.
Mkutano huu pia ulionesha kupiga hatua baada ya Mataifa hayo kupunguza
makali ya Vikwazo kwa dhidi ya Iran hasa vya biashara ambavyo vilikuwa
vikiiathiri Iran kiuchumi, huku ikiitaka Iran kutazama upya Mradi wake
wa urutubishaji wa Madini ya uranium.
Iran imesema itakutana tena na Mataifa hayo nchini Kazakhstani Tarehe 5-6 Mwezi Aprili.
Via kiswahili.rfi.
Comments