Na Victor Melkizedeck Abuso
Marekani inasema Ubalozi wake mjini Kigali nchini Rwanda unajiandaa
kumsafirisha Jenerali Bosco Ntaganda aliyejisalimisha kwenye ubalozi
wake na kwamba wana matumaini kupata ushirikiano toka kwa serikali ya
Rwanda.
Bosco Ntagannda
Bosco Ntaganda aliishangaza dunia juma hili baada ya kujisalimisha
mwenyewe kwenye ubalozi wa Marekani nchini Rwanda akitaka msaada wa
kufikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC.
Msemaji wa kundi la M 23 linalowakilishwa na Askofu Jean Marie Runiga,
Salomon Baravuga amesema kiongozi wake ndiye aliyemshawishi Ntaganda
kujisalimisha huku akikanusha kundi lake kuwa na uhusiano na kiongozi
huyo.
Kwa upande mwingine msemaji wa kisiasa wa kundi la M23 linaloongozwa na
Sultan makenga, Betrand Bisimwa ameendelea kusisitiza kuwa Runiga na
kundi lake walikuwa na uhusiano wa karibu na Ntaganda waliyetaka arejee
katika kundi lao.
Rais Joseph Kabila ameendelea kukutana na viongozi mbalimbali nchini
humo kujadili hali ya amani Mashariki mwa nchi hiyo huku baada ya
Ntaganda kujisalimisha.
Ntaganda anatuhumiwa kuongoza makundi kadhaa ya uasi Mashariki mwa nchi
hiyo kabla ya kupewa cheo katika jeshi la serikali kaa njiamojawapo ya
kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo.
Comments