Rais wa zamani wa Cote d Ivoire atoa utetezi wake katika mahakama ya ICC kuwa alikuwa akipigania Demokrasia nchini mwake
Kiongozi wa zamani wa Cote d ivoire, Laurent Gbagbo |
Na Lizzy Anneth Masinga
Rais wa zamani wa Cote d Ivoire, Laurent Gbagbo ameiambia Mahakama ya
kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC kuwa siku zote amekuwa akiunga mkono
Damokrasia nchini mwake.
Gbagbo ameiambia mahakama ambayo huenda ikamfungulia mashtaka au la
Kiongozi huyo wa zamani kutokana na makosa ya uhalifu wa kivita iwapo
itajiridhisha.
Gbagbo,67 ni Kiongozi wa kwanza wa zamani kufikishwa katika Mahakama ya
kimataifa ambapo anashutumiwa kufanya kampeni kuchochea machafuko wakati
wa Uchaguzi wa nchini Cote d Ivoire.
Gbagbo anakabiliwa na Makosa manne ya uhalifu dhidi ya ubinaadam wakati
na kuzuka kwa Machafuki makubwa alipokaidi kuondoka madarakani na
kumpisha Mshindi wa uchaguzi huo, Allasane Ouattara baada ya kuwepo
madarakani kwa kipindi cha miaka 10.
Kati ya tarehe 28 mwezi November 2010 na Tarehe 8 mwezi May mwaka 2011,
Vikosi vya Gbagbo viliua takriban watu 1000 na kuwabaka Wanawake zaidi
ya 35.
Via kiswahili.rfi.fr
Comments