Shindano la Taifa la Miss Utalii Vipaji 2012/13 linafanyika kesho katika ukumbi wa Dar Live Mbagala, ambapo Warembo 40 kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na Kanda Maalum vyuo Vikuu Tanzania , watapanda stejini kushindana kucheza Ngoma za asili kutoka Mikoa ambayo wanawakirisha,watapita na mavazi mbalimbali.
Katika shindano hilo mbali na Burudani kutoka kwa Warembo wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutakuwa na Burudani zaidi za Ngoma za Asili, Muziki wa kizazi Kipya pamoja na Burudani kutoka kwa Mwanamuziki wa Kimataifa Che Mundugwao, Atakuwepo pia mwanamuziki chipukizi wa Bongo Flava Dogo Genius ambeye ametokea kuwa mpinzani mkubwa wa Dogo Janja na Asley.
Comments