Lionel Messi, mchezaji wa Barcelona aliyepachika mabao mawili katika mechi dhidi ya AC Milan
Klabu ya Barcelona ya Uhispania imedhirisha msemo wa waswahili kuwa
kutangulia sio kufika baada ya kufuzu katika robo fainali ya michuano ya
ligi ya mabingwa kwa kuigaragaza AC Milan ya Italia mabao 4 kwa 0 jana.
Mashabiki wa Barcelona watamkumbuka sana Lionel Messi ambaye aliifungia Barcelina mabao mawili katika mchuano huo.
Wengi walikuwa wametabiri kuwa huenda Barcelona wangetolewa nje ya
michuano hiyo baada ya kufungwa na AC Milan mabao 2-0 katika mchuano wa
kwanza waliocheza ugenini mwezi uliopita.
Mabao mengine ya Barcelona yalipachikwa na David Villa aliyefunga la
tatu katika dakika ya 55 huku Jordi Alba akifunga bao la mwisho katika
dakika za lala salama la mchuano huo.
Via kiswahili.rfi.fr
Comments